UMEONA JINSI KABURI LA MAITI ILIYOZIKWA NA KUKU BAADA YA TUMBO KUCHANWA WEMBE LILIVYOFUKULIWA SHINYANGA? ZIKO HAPA
Siku
10 tu baada ya marehemu Benadetha Steven(35) aliyefariki kutokana na
uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala katika
manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kuzikwa na kifaranga cha kuku
tumboni kwa madai kuwa ndugu wanaondoa mikosi katika familia,kaburi lake
limekutwa limefukuliwa na watu wasiojulikana,malunde1 blog inakupa
mkasa mzima.
Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za nyayo za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika kaburi hilo.
Walioshuhudia
tukio hilo walisema taarifa za kuwepo kwa tukio hilo la kushangaza
zilienea Siku ya Jumatatu Januari 12,2015 jioni na kesho yake Jumanne
Januari 13,2015 asubuhi uongozi wa eneo husika ulifika katika makaburi
ya kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga alikozikwa marehemu
huyo na kukuta halisi jinsi kaburi lilivyokuwa limefukuliwa.
Mmoja
wa mashuhuda hao Makaranga Mabula(60) alisema tukio hilo linatokana na
imani za kishirikina na kwamba tukio la kufukua kaburi ni kwanza kutokea
katika kata ya Ndala hivyo kuviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi
ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo la kinyama.
Mjumbe
wa serikali ya mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo alikozikwa marehemu
Josephine Kishiwa (Chadema)alisema alipokea taarifa za kuwepo kwa tukio
hilo siku ya Jumatatu saa moja usiku na kesho yake asubuhi alikwenda
kwenye kaburi hilo akiwa na wanamtaa wengine na kukuta kweli kaburi hilo
limefukuliwa.
“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na sanda
ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na
binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa
kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi
hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”,alisema Kishiwa
aliopozungumza na Malunde1 blog.
Naye
mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala(Chadema)
Deogratius Masanja alisema kwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka mume
wa marehemu Maulid Omari Njunju ambaye hakutaka kuzungumza na waandishi
wa habari,alidai kuwa siku tatu zilizopita ndugu wawili wa marehemu walionekana katika mtaa huo katika mazingira ya kutatanisha.
“Huenda
ndugu wa marehemu wamehusika,kwani mume anasema ndugu walionekana hivi
karibuni kuja kumalizia kufanya mambo yao ya kimila wakati wa mazishi
Januari 3,2015,kaburi limefukuliwa liko juu,huenda hata mwili wa
marehemu umechukuliwa”,Masanja aliiambia Malunde1 blog.
Hata
hivyo kuna taarifa kuwa juzi nyakati wakati wa usiku watu wasiojulikana
wakiwa na gari walionekana eneo la makaburi hivyo kuleta sintofahamu
kama ni ndugu wa marehemu ama watu wengine wamehusika katika tukio hilo.
Kufuatia
taarifa hizo saa 6 mchana Januari 13,2015 jeshi la polisi lilifika
katika kaburi la marehemu na kuuomba uongozi wa eneo husika kuruhusu
kaburi la marehemu lifukiwe kwani jeshi la polisi halina na mamlaka ya
kufukua mwili bali mahakama ndiyo yenye mamlaka hayo.
Akizungumza
katika eneo la tukio mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman
Taibu alisema wanalaani tukio hilo linalohusishwa na imani za
kishirikina na kukosa hofu ya mungu huku akiwataka wananchi kumrudia
mungu na kuwafichua watu wote wanaofanya uhalifu.
“Hili kaburi halijatitia,hii ni
tabia mbaya sana,hatuwezi kuvumiliana kwa hali hii,unatafuta nini
kwenye kaburi la marehemu,unachukua nini kwa ajili ya nini,nawashauri
wananchi kuwa walinzi wa kila mmoja,toeni taarifa za mnayehisi kafanya
jambo hili kwa viongozi wenu sisi tutajua cha kumfanya”,alisema Taibu.
Mkuu
huyo wa upelelezi mkoa wa Shinyanga alisema jeshi la polisi halina
mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali mahakama pekee ndiyo yenye
yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi kufukuliwa hivyo kuwaomba
wananchi kufukia kaburi hilo badala ya kulifukua.
“Naomba
mrudishie udongo,sababu ya kufukua kaburi hatuna,tunatafuta nini kwa
marehemu,tunachoamini ndugu yetu alikufa kifo cha kawaida,na alizikwa
kawaida,haya mambo yaliyojitokeza ya mila siyo sahihi,ni mila potofu na
hazifai kwa jamii,ndiyo maana tunasema ni bora watu wamwamini mungu ili
waachane na mila hizi za kishirikina”,aliongeza Taibu.
Kitendo cha kaburi la marehemu kufukiwa bila kufukuliwa kimezua maswali kwa wakazi wa eneo hilo huku wengine wakisema kuwa ni bora kaburi lingefukuliwa kwa hivi sasa hawaamini kama mwili wa marehemu upo kaburini au la kutokana na sanda na jeneza kuonekana juu sana tena kama limetobolewa na udongo kwenye kaburi hilo kuonekana kupungua ukilinganisha na ulivyokuwa siku ya mazishi.
Kitendo cha kaburi la marehemu kufukiwa bila kufukuliwa kimezua maswali kwa wakazi wa eneo hilo huku wengine wakisema kuwa ni bora kaburi lingefukuliwa kwa hivi sasa hawaamini kama mwili wa marehemu upo kaburini au la kutokana na sanda na jeneza kuonekana juu sana tena kama limetobolewa na udongo kwenye kaburi hilo kuonekana kupungua ukilinganisha na ulivyokuwa siku ya mazishi.
Benadetha
Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki
dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali
ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo
mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani
Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe
kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye
tumbo la marehemu.
Kitendo
hicho ambacho ndugu wa marehemu walidai wanaondoa mikosi kwenye familia
baada ya kudai wanafamilia wengine kufa kwa ugonjwa wa namna
hiyo,waombolezaji waliondoka makaburini wakidai kuwa kitendo cha
marehemu kupasuliwa tumbo tena kwa wembe hadharani ni cha fedheha.
Hata
hivyo ndugu wa marehemu hawakujali waliendelea kuzika na baadaye
kukamatwa na polisi kwa muda na kuhojiwa kisha kuruhusiwa kuzika ndugu
yao huku waombolezaji wachache wakijitokeza kujumuika na ndugu wa
marehemu kumzika marehemu.
Na Kadama Malunde-Shinyanga