Kauli ya Zitto Kabwe kuhusu Kurudi tena CHADEMA


 Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa 2014 kulikuwa na mgogoro kati yake na Chama cha CHADEMA.
 
Magazeti  mengi yaliyotoka siku chache zilizopita yaliripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena CHADEMA, hali  iliyomfanya  Zitto  afunguke  kuhusiana  na  ishu  hiyo.
 
Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa,bado inaendelea.
 
Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa CHADEMA, mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi, inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua, hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo“– Zitto Kabwe.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini