Mwandishi aliyetuhumiwa kwa Rushwa aachiwa huru
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, jana imemwachia huru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Rai, Masyaga Matinyi baada ya kushindwa kumtia hatiani dhidi ya tuhuma za kupokea rushwa zilizomkabili yeye na wenzake watatu.
Pia Mahakama hiyo imemtia hatiani mtuhumiwa wa pili Mwita Chomete na
kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Shilingi laki
tatu.
Katika kesi hiyo ya Mwaka 2012 mlalamikaji alikuwa Andrew Meza
akisaidiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), dhidi
ya Matinyi, Chomete na Bora Bidige wanaodaiwa kushawishi na kupokea
rushwa wilayani Monduli mkoani Arusha.
Akisoma hukumu hiyo mapema leo, Hakimu wa mahakama hiyo, Gwantwa
Mwankuga amesema, katika kosa la kwanza Mahakama, imeshindwa kuwatia
hatiani watuhumiwa wote kutokana na upande wa mlalamikaji kuwasilisha
ushahidi mwepesi.
Katika upande wa walalamikaji waliwasilisha mashahidi Saba, huku
mashahidi katika shitaka la kushawishi wakiwasilisha ushahidi wa
mawasiliano ya simu ambayo yalidaiwa kuwa si rasmi kutoka kwenye mamlaka
zinazohusika na mawasiliano.
Kutokana na uamuzi huo Mahakama hiyo iliwakuta hawana hatia
watuhumiwa wote watatu, katika kosa hilo la kwanza hivyo kuwaachia huru
Matinyi, Chomete na Bigide.
Akisoma shitaka la pili liliwakabili pia watuhumiwa wote Hakimu
Gwantwa, amesema, mtuhumiwa wa pili Chomete alikutwa na hatia katika
kosa hilo kutokana na ushahidi wa mashahidi wa kwanza na wa pili kueleza
kuwa alipokea rushwa ya fedha.
Amesema katika ushahidi wa mashahidi wa kwanza na wa pili, wameeleza
kwamba mtuhumiwa wa pili alipokea fedha japo hawakuthibitisha zilikuwa
ni fedha za nini.
Gwantwa amesema kwa maana hiyo, kitendo cha fedha kutupwa nje
kinathibitisha wazi kwamba fedha ilitolewa ndani. hivyo Mahakama imemtia
hatiani kwa kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya Shilingi laki
tatu.
Hata hivyo mtuhumiwa wa pili Chomete aliyekutwa na hatia, amelipa faini ya Shilingi laki tatu na kuachiwa huru.
Katika kesi hiyo Matinyi alikuwa akitetewa na Wakili Mwandamizi wa
jijini Arusha Moses Mahuna, kutoka Kampuni ya Law Acces Advocates.
Akizungumzia mara baada ya kushinda kesi hiyo nje ya mahakama hiyo,
Matinyi amemshukuru Mungu na kumpongeza wakili wake kwa kumpigania