MAKINDA AONGOZA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE, KIKAO CHA BUNGE KUANZA JANUARI 27

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi wakati kamati hiyo ilipokaa kuapanga ratiba ya Mkutano wa Bunge kwenye ofisindogo za bunge jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Januari 22, 2015. Kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza Januari 27, 2015
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza kamati Uongozi leo
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajabu Mbarouk akieleza jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi wakati kamati hiyo ilipokaa kuapanga ratiba ya Mkutano wa Bunge unaoanza jumanne tarehe 27 Januari

Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unatarajiwa kuanza Jumanne tarehe 27
Januari 2015 mjini Dodoma na kumalizika tarehe 7 Februari 2015 Shughuli zitakazokuwepo katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:


1.0 KIAPO CHA UTII
Kwa mujibu wa Kanuni ya 24, katika Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge kutakuwa na Kiapo cha Utii kwa Mbunge ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, (Mb) ataapishwa baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Mwita Werema.

2.0 MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:
Aidha, kwa Mujibu wa Kanuni ya 86 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jumla ya Miswada Mitatu (3) itasomwa na kupitishwa na Bunge. Miswada hiyo ni:
2
(i) Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014] (Kupigiwa kura tu).
(ii) Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013[ The Statistic Bill, 2013] (Kamati ya Bunge zima na Kusomwa mara ya Tatu)
(iii) Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill, 2014]

3.0 TAARIFA ZA CAG:
Pamoja na Miswada hiyo, Bunge pia litajadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka 2012/2013, ambapo pia
Serikali itatolea majibu baadhi ya Hoja.

4.0 TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE
Kwa kuzingatia Kanuni ya 117 (15) katika Mkutano wa 18 wa Bunge, Kamati za Bunge zitapewa nafasi ya kuwasilisha Taarifa za Mwaka za Shughulii za Kamati na zitapangiwa muda wa kujadiliwa kwa kadri Spika atakavyoelekeza.

5.0 TAARIFA YA KAMATI TEULE
Aidha, Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, Kilimo, Mifugo Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matuymizi ya Ardhi itapewa nafasi ya kuwasilisha Taarifa yake, ambapo taarifa hiyo itajadiliwa Bungeni.
3

6.0 MASWALI:
Jumla ya Maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa ambapo ni wastani wa Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku za Alhamisi. Aidha katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuuinatarajiwa kuwa jumla ya Maswali 18 ya msingi yataulizwa na kujibiwa na Mhe.
Waziri Mkuu. Aidha, Kamati ya Uongozi imefikira pia ratiba ya Mkutano wa kumi na tisa (19)
na Ishirini (20) ambapo imependekezwa kuwa Mkutano wa Kumi na tisa utajadili Miswada yote ya Serikali iliyosomwa kwa mara ya kwanza na miswada mingine itakayoonekana kuwa na umuhimu kabla ya Bunge kuvunjwa. Mkutano huo wa Kumi na Tisa utafanyika tarehe za Katikati ya Mwezi Machi na Kumalizika Mwanzoni mwa Mwezi Aprili, ambapo Mkutano wa Ishirini wa Bajeti
utafanyika tarehe za Mwanzoni mwa mwezi Mei na kumalizika tarehe 30 Juni 2015.
Ratiba Kamaili ya Mkutano wa Kumi na Nane (18) ya jinsi shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa mapema na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz
Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,

Ofisi Ndogo za Bunge
DAR ES SALAAM
22 Januari 2015

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini