MGOMO WA WAENDESHA DALADALA JIJINI MWANZA
Daladala zikiwa zimepaki katika Jiji la Mwanza kutokana na mgomo wa madereva.
WAENDESHA magari ya kusafirisha abiria katika ya Jiji la Mwanza
maarufu kama daladala leo wamefanya mgomo na kuziba njia zote
zinazoingia mjini kutokana na maeneo waliyokuwa wanaegesha magari yao
kwa ajili ya kusubiri abiria (stendi) kugawiwa wafanyabiashara
ndogondogo maarufu kwa jina la machinga kwa aijili ya shuhuli zao.
Hali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Stendi ya Tanganyika na
Stend ya Soko Kuu jijini Mwanza ambapo yanaegesha magari ya kwenda
Airport, Ilemela, Bwiru na Mwaloni ambapo madereva hao waliziba njia
zote zinazo ingia kwenye maeneo hayo.
Mwenyekiti wa waendesha daladala Mkoani Mwanza, Hassan Dede Petro
alisema hali hiyo imejitokeza kutokana na wafanyabiashara hao kuanza
kugawana maeneo kwenye stendi hizo bila uongozi wa waendesha daladala
kuwa na taarifa yeyote kuhusu suala hilo.
''Hali hii imejitokeza kwa sababu ya wafanyabiashara wadogodogo
kuanza kujigawia maeneo katika eneo letu ambalo tunaegesha kwa ajili ya
kusubiri wateja wetu (abiria)'' Alisema Petro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo 'machinga'
Said Tembo alisema walichukua uamuzi huo kutokana na kupata ruhusa
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Magesa Mulongo kuwa watumie
maeneo hayo kwa shuhuli zao za kufanyabiashara kwenye maeneo ya stendi
hizo.