POLISI WATANGAZA MBINU MPYA YA KUMTAFUTA MTOTO ALBINO ALIYETEKWA JIJINI MWANZA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola akionesha picha ya mtoto Pendo Emmanuel (4) aliyetekwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Ndami, wilayani Kwimba kwa waandishi wa habari jijini Mwanza juzi ili kuwezesha yeyote atakayemwona kutoa taarifa Polisi ama kwenye ofisi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. (Picha na Grace Chilongola).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola akionesha picha ya mtoto Pendo Emmanuel (4) aliyetekwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Ndami, wilayani Kwimba kwa waandishi wa habari jijini Mwanza juzi ili kuwezesha yeyote atakayemwona kutoa taarifa Polisi ama kwenye ofisi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. (Picha na Grace Chilongola). 
POLISI mkoani hapa imetoa picha ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel (4) aliyetekwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Ndami, wilayani Kwimba ili kuwezesha yeyote atakayemwona kutoa taarifa Polisi ama kwenye ofisi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Picha hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya matukio mbalimbali ya uhalifu.
Alisema mtoto Pendo aliporwa na watu wasiojulikana kwa kuvamia makazi yao usiku wa Desemba 27, mwaka jana akiwa amelala pamoja na wazazi wake na kisha kupora mtoto huyo na kutokomea kusikojulikana.
“Natoa wito kwa yeyote atakayemwona mtoto huyo atoe taarifa katika kituo cha Polisi ama kwenye ofisi za serikali za mitaa, vijiji na vitongoji,” alisema Kamanda Mlowola.
Kamanda Mlowola alisisitiza kuwa Polisi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa imeimarisha juhudi za kumsaka mtoto huyo na kuomba wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alitembelea kijiji hicho Januari 5, mwaka huu na kuzungumza na wakazi wa kijiji hicho ambao alitoa siku tano mtoto huyo awe amepatikana akiwa hai ama mwili wake lakini hadi sasa mtoto huyo bado hajapatikana.
Baba wa mtoto Pendo, Emmanuel Shilinde ni miongoni mwa watu wanoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ya namna mtoto huyo alivyoporwa na watu wasiojulikana.
Watu 15 wenye ulemavu wa ngozi wameuawa mkoani Mwanza tangu kuibuka kwa wimbi la mauaji dhidi yao nchini mwaka 2008 kutokana na imani za kishirikina.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …