WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO WAKATI WAKIIBA SARUJI KWENYE LORI


Zaidi ya watu 50 wamenusurika kifo katika ajali ya moto wakati wakijaribu kupora saruji kwenye gari la mizigo lililopasuka tairi moja ya mbele na kusababisha mlipuko mkubwa wa moto kwenye tenki la kuhifadhi mafuta baada ya kushindwa kuzima moto ulioteketeza gari hilo sehem ya mbele katika kijiji cha Nterungwe wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Gari hilo lililokuwa likitoka mkoa wa Tanga kuelekea nchi ya Burundi kupitia Kabanga wilaya ya Ngara mkoani Kagera limepata ajali hiyo majira ya saa moja na dakika 30 za usiku.
 
Dereva wa gari hilo amesema kuwa baada ya gari kupata hitilafu ya kuwaka moto aliomba msaada kwa wananchi ambao walijaribu kuzima gari kwa mchanga na maji bila mafanikio ndipo likaibuka kundi la watu kupora saruji baada ya jeshi la polisi kuchelewa kufika kwenye eneo la tukio.

Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi linawashikilia watu kumi kwa tuhuma ya wizi na gari tatu zilizokamatwa zikiwa na saruji za wizi ambapo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu amewataka wananchi kuacha tabia ya kupora vitu kwenye ajali kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Wilaya ya ngara iliyopo pembezoni mwa mkoa wa Kagera inapakana na nchi ya Burundi na Rwanda inakabiliwa na changamoto mbalinbali za miundombinu ikiwemo ukosefu wa gari ya kuzima moto, hali inayohatarisha maisha ya watu pindi kunapotokea majanga ya moto.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini