Boko Haram:Nchi za Ulaya zakosolewa

Kiongozi wa kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likifanya mashambulizi kila kukicha nchini Nigeria
Askofu mmoja nchini Nigeria ametoa wito kwa mataifa ya magharibi kufanya juhudi za kutosha dhidi ya Boko Haram kama ilivyofanywa dhidi ya washambuliaji wa kiisilamu nchini Ufaransa.
Askofu Ignatius Kaigama amesema mataifa ya magharibi yanapuuza sana tisho linalotokana na Boko Haram kwa watu wa Nigeria.
Askofu huyo wa Jos, aliongeza kwamba rasilimali zote zinatakiwa kutumika ili kuzuia juhudi za kundi hilo kukita mizizi nchini Nigeria. Pia amesema kwamba dunia inapaswa kuonyesha ari ya kutaka kuangamiza kundi hilo.
Kadhalika askofu huyo amesisitiza kwamba mauaji ya hivi karibuni ya mamia ya watu mjini Baga ni ishara kwamba jeshi la nchi hio limeshindwa kukabiliana na wapiganaji hao.
Onyo la askofu huyo linakuja siku mbili tu baada ya mashambulizi ya bomu kuwaua zaidi ya watu 20.
Mnamo Jumapili,washambuluaji wawili wa kike walifanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na kuwaua watu wanne huku wnegine zaidi ya arobaini wakijeruhiwa mjini Potiskum
Siku moja kabla ya mashambulizi hayo, mashambuluaji mwingine w akujitoa mhanga alishambulia mji wa Maiduguri na kuwaua watu 19.
Mashambulizi haya yametokea baada ya taarifa kwamba mamia ya watu waliuawa wiki jana wakati Boko Haram ili poteka mji wa Baga katika jimbo la Borno.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini