WANAFUNZI 150 WA CHUO KIKUU CHA DUCE WADUNGWA MIMBA
Wanafunzi 150 kati ya 1,000 waliojiunga na masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) mwaka jana wamebainika kuwa na ujauzito waliopewa na wenzao chuoni hapo.
Utafiti wa usawa na jinsia uliofanywa na chuo hicho kati ya Juni na
Novemba mwaka jana umebaini kuwa wanafunzi wanaopata ujauzito ni wale wa
mwaka wa kwanza.
Hayo yamebainishwa jana na Mratibu wa
Masuala ya Jinsia wa chuo hicho, Dk Dativa Shilla katika warsha ya
uchaguzi na uhusiano wa kijinsia iliyofanyika chuoni hapo na kusema hali
hiyo inatokana na kuwapo kwa vitendo vya ukatili, manyanyaso na ubabe
unaofanywa na wanachuo wa kiume dhidi ya wale wa kike na hivyo
kuwalazimisha kufanya mapenzi bila hiyari yao.
“Kupitia utafiti huu tumeona hakuna
usawa wa kijinsia wa kupata elimu baina ya mwanamke na mwanamume kwa
sababu mwenye ujauzito hawezi kufanya vizuri katika masomo yake
ukilinganisha na mhusika wa kiume,” alisema.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho Gosbeth Kihanga ambaye alikiri kuwapo kwa vishawishi chuoni hapo na kudai kuwa inachangiwa na ugumu wa maisha hasa kwa wanafunzi wa kike.