AMUUA MPENZI WAKE NA KUMZIKA KWENYE BUSTANI YA MBOGA!

Mwanaume mmoja kutoka Mpumalanga, Afrika Kusini amepandishwa kizimbani  katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkobola kwa kosa la kumuua mpenzi wake na kumzika katika bustani iliyo nyuma ya nyumba yake. 

Tukio la kupotea kwa mwanamke huyo liliripotiwa katika kituo cha Polisi siku ya Jumapili January 4, siku iliyofuatia Polisi walianza na upelelezi wa tukio hilo, mwanaume huyo alihojiwa, alipoulizwa kuhusu mahali alipo mwanamke huyo ambaye alikuwa ni mpenzi wake, alijibu kwamba hajarudi nyumbani hapo tangu alipoaga kwenda kutoa pesa Benki. 

Ukaguzi ulipokamilika ndani ya nyumba Polisi walihamia nje wakagundua kuna udongo unaoonyesha kuchimbwa siku za karibuni, alipoulizwa alichimba kwa ajili ya nini akasema alikuwa analima. 

Polisi walitilia shaka maelezo yake, wakaagiza iletwe koleo ili wachimbe, jamaa huyo akakiri kwamba ni kweli kamuua mpenzi wake na kumzika katika bustani hiyo.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini