Jeshi la Polisi limekamata shehena ya nyaya za umeme kwenye nyumba ya mkazi mmoja eneo la Nyeburu wilayani Ilala.


Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo limekamata shehena ya nyaya za umeme kwenye nyumba ya mkazi mmoja eneo la Nyeburu kata ya Majohe wilayani Ilala.
Hatu ya kukamatwa na nyaya hizo imetokana na baadhi ya wasamaria wema kuiarifu polisi baada ya kutilia shaka roli moja lililobeba nyaya hizio katika nyumba ya mkazi huyo na kusafirishwa na ndipo polisi ilipofika na kufanya ukaguzi ikazikuta rundo hilo huku mhusika akikimbia na kuacha familia yake.
 
Meneja wa shirika la ugavi la umeme tawi la kisarawe madaraka marumbo amesema ni wizi mkubwa ambao unashangaza kuona vifaa vilivyokutwa hapo ni vingi vyenye kama ghala huku ikiwa na thamani isiyopungua milioni 100 ambayo vinaweza kupelekwa kwenye mradi wowote.
 
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Nyeburu Bw,Hamisi Gea amesema aliitwa na polisi waliokuwa wakitaka kufanya upekuzi na alishangazwa kuona mkazi huyo ana rundo la vifaa hivyo.
 
Hadi ITV ikiondoka eneo hilo tayari roli tatu za Tanesco ikiwamo winchi ilikuwa ikipakia vifaa hivyo kwa ajili ya kuvipeleka polisi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini