MWANAMKE AMCHOMA MOTO MTOTO WAKE KATIKATI YA BARABARA BAADA YA KUJIFUNGUA

new jMwanamke nchini Marekani anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji baada ya kuamua kumweka mtoto wake aliyetoka kujifungua katikati ya barabara kisha kumchoma moto.
Mwendesha mashtaka aliyekua akisimamia kesi hiyo alisema mwanamke huyo Hyphernkemberly Dorvilier anashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Polisi walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto huyo akiteketea kwa moto katikati ya barabara ya makazi ya watu ambayo ni maili 30 kutoka jiji la Mashariki mwa mji wa Philadelpia na kumkimbiza katika hospitali ya St. Christopher lakini alifariki masaa mawili baada ya tukio hilo.
Mashahidi walisema walimwona mama huyo akichoma kitu lakini hawakujua ni nini na walipomuuliza alisema alikuwa akichoma uchafu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini