WATOTO WAANDAMANA, POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA

Askari Polisi wa Kenya katika mji mkuu Nairobi leo wamewafyatulia mabomu ya machozi wanafunzi wa shule ya msingi Lang’ata waliokuwa wakiandamana kupinga kunyang’anywa ardhi ambayo ilikuwa kiwanja chao cha michezo.
watoto2
Polisi hao wakiwa na mbwa waliwatawanya wanafunzi ambao wengi wao inasemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuangusha ukuta mpya uliojengwa katika eneo la shule.
watoto3
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogo madogo huku polisi mmoja akiumizwa baada ya kupigwa jiwe usoni na wanafunzi.
Hii imetokea leo January 19, siku ambayo wanafunzi hao walifika shule kwa mara ya kwanza baada ya mgomo wa walimu uliokuwepo kwa wiki mbili kutokana na madai yao ya mishahara.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini