MWANASHERIA NA WAKILI MAARUFU APANDISHWA KIZIMBANI ARUSHA KWA MAKOSA 42

MWANASHERIA na wakili maarufu wa kujitegemea wa jijini hapa, Medium Mwale anayemiliki kampuni ya uwakili ya JJ Mwale Advocates na wenzake watatu jana walisomewa mashitaka mapya 42 ya utakatishaji fedha haramu, kula njama na kughushi baadhi ya nyaraka na kujipatia kiasi cha Sh bilioni 18.
Mbali ya Mwale wengine walioshitakiwa na mwanasheria huyo ni pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mapato jijini Arusha, Boniface Thomas mwingine ni mfanyabiashara wa jijini Nairobi, DonBosco Gichana, Bob James Onderi na Elias Ndejembi.
Katika kesi ya msingi iliyosomwa Agosti, 2011, Mwale na wenzake walisomewa mashitaka 30 na wakili mwandamizi wa Serikali, Frederick Manyanda na ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo na wenzake wanatuhumiwa kujipatia zaidi ya Sh 18 kwa njia haramu ya utakatishaji fedha haramu ikiwa ni pamoja na kughushi nyaraka na kuhujumu uchumi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini