Jeshi la polisi ladhibiti wananchi waliotaka kuiba mafuta baada ya lori kuanguka, Morogoro


Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wanachi waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
 
Dereva wa lori Deogras John hilo akizungumzia tukio  hilo la ajali amesema chanzo cha ajali alikua akijaribu kumkwepa mtoto aliyekua akivuka barabara ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo wananchi walijitokeza na madumu na kuanza kuiba mafuta.
 

Nao wananchi wa eneo la Mikese katika hali isiyo ya kawaida wamelalamikia jeshi la polisi  kuwazuia kuiba mafuta na kueleza kuwa wamefanya kazi ya kumuokoa dereva kwa kumtoa kwenye gari na hivyo walipaswa kuchukua mafuta kama ujira wao.

WEKA MAONI YAKO HAPA

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini