Mapacha wa Miaka 6 wafa Maji kisimani

Watoto mapacha wenye umri wa miaka sita, wamekufa baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati wakicheza.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema watoto hao  walitumbukia kwenye kisima kilicho jirani na nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, tukio hilo ni la juzi saa 10 jioni katika Kijiji cha Pipani – Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa tarafa ya Msata wilaya ya Bagamoyo.


“Pacha wa kwanza alipoona mwenzake amezama, alikwenda na kutaka kumwokoa mwenzake ndipo naye alipozama,” alisema Kamanda Matei na kuongeza kwamba miili yao ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini