AUNTY EZEKIEL Azua Minong’ono Ukumbini Usiku!
STAA wa kiwango cha juu kupitia filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, kwa mara ya kwanza tangu ajifungue, amezua minong’ono ukumbini.
Mpango mzima ulishuhudiwa na gazeti hili usiku kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, Zanzibar ambapo kulikuwa na Tamasha la Kimataifa la Filamu (ZIFF) ambapo Aunt alitinga akiwa na baadhi ya mastaa wenzake huku baadhi ya watu wakishangaa na kunong’ona kuwa mtoto wake bado ni mdogo iweje awe ukumbini badala ya kuwa naye muda huo.
“Mmmmh huyu siyo Aunt kweli? Jamani mtoto wake mbona bado mdogo sana kwa nini amekuja ukumbini usiku wote huu?” alihoji mmoja wa watu waliokuwa ukumbini humo.
Amani lilipozungumza na Aunt kuhusiana na minong’ono hiyo alisema: “Niko makini san-a kwa upande wa mtoto, hapa nilipo nikitoka nje tu naona hoteli niliyofikia na mwanangu hivyo hakuna shida na siwezi kuja na mtoto hapa kwenye mkusanyiko wa watu wengi,” alisema Aunt.