Stori ya mwanamke kuripotiwa kufa na baadaye kukutwa hai isikupite mtu wangu…
Kuna stori moja iliwahi kuripotiwa na kipindi cha HekaHeka maeneo ya Bagamoyo baada ya maiti kuzua taharuki kwa waombolezaji wakidai hajafa licha ya kudhibitishwa na daktari kuwa alifariki.
Huko Ujerumani mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 92 ambaye aliaminika kupoteza maisha kisha mwili wake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti amezua gumzo.
Tayari daktari wa zamu alithibitisha kifo cha mwanamke huyo baada ya kumpima na kuridhika kuwa amefariki ..lakini baada ya masaa machache wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti walikuta mwili wa mwanamke huyo ukijigeuza na kugundua alikua hajafariki kama ilivyoripotiwa.
Tukio hilo lilifanya ndugu wa marehemu kushangazwa na hali hiyo huku wakimjia juu daktari aliyewapa taarifa kuwa mgonjwa wao amefariki duniani na kutaka walipwe fidia.