KWANINI CHADEMA WAMEMCHUKUA LOWASSA? [Kama una AKILI NDOGO usisome]

KWANINI CHADEMA WAMEMCHUKUA LOWASSA?? 
(Kama una akili ndogo usisome) 
Mnamo mwezi February mwaka huu Umoja wa 
Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliingia ubia na 
kampuni maarufu duniani inayojihusisha na tafiti 
za siasa (Political Research) ijulikanayo kama 
Greenberg Quinlan Rosner. ( 
www.gqrr.com/ 
). 
UKAWA walitaka kujua kama wana nafasi ya 
kushinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu. 
Kampuni hiyo ilimaliza utafiti wake mwezi May 
mwaka huu na haya ndio yalikua majibu; 
1. Ikiwa CCM itamsimamisha Lowassa kugombea 
Urais, na UKAWA wakamsimamisha Dr.Slaa, CCM 
watashinda kwa 58% dhidi ya 42% za UKAWA. 
2. Ikiwa CCM itamsimamisha mgombea mwingine 
asiye Lowassa kushindana na Dr.Slaa, CCM 
itashinda kwa 54% dhidi ya 46% za UKAWA. 
3. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mgombea 
mwingine ambaye si Dr.Slaa na CCM 
ikamsimamisha Lowassa, CCM itashinda kwa 
68% dhidi ya 32% za UKAWA. 
4. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mtu mwingine 
ambaye sio Dr.Slaa na CCM ikamsimamisha mtu 
mwingine ambaye sio Lowassa CCM itashinda 
kwa 57% dhidi ya 43% UKAWA. 
5. Ikiwa watu wote wa CCM wanaotaka Urais 
wakiwekwa Pamoja na wa UKAWA wakawekwa 
pamoja kisha wapigiwe kura za Urais kama 
wagombea huru, Lowassa ataongoza kwa 14% 
kisha Dr.Slaa atafuata kwa 09%, Membe 04% na 
wengine chini ya hapo. 
6. Ikiwa Lowassa atagombea kupitia UKAWA 
atapunguza kura za UKAWA kwa 06% lakini 
ataziongeza kwa 24%. Hii ina maana kuwa katika 
watu 100 wa CHADEMA watu 6 hawataipigia kura 
CHADEMA kwa sababu hawamtaki Lowassa. 
Lakini Lowassa ataleta watu wapya 24. Yani 
CHADEMA itapoteza kura 6 za wanachama wake 
lakini itapata kura mpya 24 mpya. 
DATA ANALYSIS 
Ukisoma vzr huo utafiti hapo juu utagundua kuwa 
Lowassa anaongeza umaarufu wa CCM kwa 18%. 
Kwa hiyo kuondoka kwa Lowassa kutaipunguzia 
nguvu CCM kwa 18%. 
Sasa ikiwa CCM yenye Lowassa ina nguvu 58% 
na UKAWA yenye Dr.Slaa ina nguvu 42%, maana 
yake ni kwamba kumuondoa Lowassa CCM ni 
kupunguza nguvu yao kwa 18% yani (58-18) = 
40%. 
Na kumleta Lowassa UKAWA ni kupunguza nguvu 
ya UKAWA kwa 6% lakini kuongeza kwa 24%. Kwa 
hiyo chukua 42 toa 06 kisha jumlisha 24 utapata 
60%. 
Sasa jumlisha 40% za CCM na 60% za UKAWA 
kama haiji 100%?? 
Kwa hiyo UKAWA yenye Lowassa inashinda 
uchaguzi kwa nguvu kubwa zaidi kuliko ambavyo 
CCM ingeshinda ikiwa na Lowassa. Na hii ni kwa 
sababu ujio wa Lowassa utaivunja CCM vipande 
vipande. 
Na ili uweze kuishinda CCM lazima uivunje 
vipande kwanza. Huwezi kuishinda CCM ikiwa 
imesimama imara. 
Nchini Kenya KANU ilishindwa kirahisi baada ya 
kuvunjwa vipande, Zambia UNIP ilishindwa baada 
ya kuvunjwa vipande, na nchi nyingine za Afrika 
vivyo hivyo. 
Na njia rahisi ya kukivunja chama tawala ni kwa 
kuondoa watu wenye ushawishi ktk chama hicho. 
Fredrick Chiluba alikua mtu mwenye ushawishi 
mkubwa akiwa UNIP lakini alipoondoka kwenda 
MMD huo ndio ukawa mwisho wa UNIP maana 
alikua na ushawishi na aliondoka na kundi kubwa 
la watu. 
Nchini Kenya akina Najib Balala, George Saitoti, 
Musalia Mudavadi, Raila Odinga, Mwai Kibaki etc 
walikua watu wenye ushawishi sana ndani ya 
KANU. Lakini walipoondoka kwenda NARC hiyo 
ndio ikawa mauti ya KANU. 
Hii ni kwa sababu watu hawa walipoondoka, 
waliondoka na kundi kubwa la wafuasi. Hivyo 
basi hata Lowassa atasaidia kuivunja CCM na 
hatimaye kuiwezesha UKAWA kushinda kirahisi. 
Ikumbukwe Nyerere aliwahi kusema huwezi 
kuishinda CCM imara yenye umoja. Kwa hiyo njia 
rahisi ya kuishinda CCM ni kuivunja vunja 
vipande. Na tayari kazi hiyo imeanza rasmi. 
BAADA YA UTAFITI. 
Baada ya ripoti ya utafiti huo wa GNR mnamo 
mwezi May, UKAWA walikaa na kutafuta njia ya 
kufanya. Walijua wazi CCM ikimpitisha Lowassa 
UKAWA itaangushwa hata imsimamishe nani. Na 
laiti CCM wangeona ripoti ya utafiti huo 
wasingefanya kosa la kumkata Lowassa. 
Wangempitisha ili waishinde UKAWA kirahisi. 
Kwa hiyo UKAWA walikua wanafuatilia sana 
mchakato wa CCM huku wakiomba usiku na 
mchana wasimpitishe Lowassa. Na kweli Mungu 
akajibu maombi yao. 
Lakini UKAWA wakatafakari ikiwa 
watamsimamisha Dr.Slaa kushindana na Magufuli 
bado UKAWA itashindwa kwa kupata 46% dhidi ya 
54% za CCM kama utafiti unavyoonesha. 
Kwa hiyo ili kuishinda CCM ni kufanya nini? Ili 
kuishinda CCM ni kumshawishi Lowassa ajiunge 
na chama kimojawapo kinachounda UKAWA ili 
apewe nafasi ya kugombea na kuiwezesha 
UKAWA kushinda. Na ndivyo ilivyotokea. 
Kwa hiyo kwa mujibu wa utafiti huo UKAWA 
itashinda kwa 60% na CCM 40% kwenye uchaguzi 
mkuu wa mwaka huu. Sasa nani asiyetaka 
ushindi? 
Siasa ni hesabu, siasa ni namba, siasa ni sayansi. 
Kama hujui hesabu usifanye siasa. 
Wavivu wa kufikiri wanaibua hoja uchwara za 
ufisadi. Hivi fisadi ndani ya CCM alikua Lowassa 
tu? Mbona baada ya kuondoka Lowassa bado 
ufisadi umeendelea kushika kasi? Escrow, 
Symbion, Meremeta, EPA etc, hivi vyote mbona 
vimefanyika bila kuwepo Lowassa? 
Acheni akili ndogo, tatizo sio mtu, tatizo ni 
mfumo. Tukibadilisha mfumo tumebadilisha kila 
kitu. Lowassa hata kama alikua fisadi kitendo cha 
kujiunga UKAWA ni rahisi kuacha ufisadi wake 
maana amejiondoa kwenye mfumo wa ufisadi. 
Lakini kumuweka Magufuli kwny kundi la mafisadi 
hata kama yeye sio fisadi lazima alinde mfumo 
wa mafisadi uliomuweka. 
Ni rahisi kumuokoa mwizi mmoja aliyeingia 
kwenye kundi la Watakatifu, kuliko kumuokoa 
mtakatifu mmoja aliyeingia kwenye kundi la 
makahaba. Mwenye masikio na asikie." 
ANGALIZO; Andiko hili nimelicopy na kupaste 
kutoka JamiiForums, kwa hiyo unapocomment 
hakikisha unazingatia kuwa haya si mawazo 
yangu wala msimamo wangu.! 
Malisa GJ

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini