Mmh..LULU Adatishwa na Picha za Ujauzito! Afunguka Kihivi...
Mkali wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Imelda Mtema
Mkali wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kudatishwa na picha za mastaa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ambao ni wajawazito kiasi ambacho zinamuhamasisha kupata mimba.
Akizungumza na Amani, Lulu alisema kuwa, picha za wajawazito kwa sasa zimeonekana kuwa na mvuto kwake zaidi, jambo ambalo linamfanya apate hamasa zaidi maana zimekuwa ndizo zenye ‘kiki’ kwa kipindi hiki.
“Picha za wajawazito kwa kipindi hiki ndizo zimekuwa zikinipata kiki halafu ni nzuri hatari na nina hofu zitawafanya watu wengi wapate ujauzito maana mimi mwenyewe kama zinataka kunibadili mawazo hivi,” alisema Lulu.