VITUKO VYA UCHAGUZI:KWELI NJIA YA MUONGO NI FUPI,DUUH..MHINDI ALIYEKAMATWA NA TAKUKURU UKONGA AKANA KUGAWA FEDHA KWA WAPIGA KURA,NIMEKUWEKEA MAELEZO ZAIDI YAPO HAPA
T888DED na T 183 CJQ ni Magari haya ndiyo yaliyohusika katika tukio zima la ugawaji rushwa huo yakiendeshwa na wapambe wa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ukonga Ramesh Patel pamoja na Prof. Felician Barongo ,Msafiri Mohamed DK, Na wengine walikamatwa na Takukuru juzi usiku katika ukumbi wa check point Pugu wakigawa rushwa kwa wajumbe wa mashina ili kuwahamaisha kumshangilia leo kwenye mkutano wa kuomba kura katika kata ya Pugu na hatimaye kumpigia kura za maoni 1/8/2015.
Ramesh na wapambe wake waliingia na magari mawili aina ya Nissan Extrail moja likimilikiwa na Prof. Barongo na lingine na Msafiri DK Magari haya ndio yanayoongozana na Ramesh toka Jumamosi kwenye kata za mzinga,kitunda,kivule na ukonga.
Baada ya Takukuru kuvamia magari hayo, na kumweka chini ya ulinzi msafiri DK na dereva aliyefahamika kwa jina la Dotto kina Barongo na wenzake walimtoa Ramesh mlango wa nyuma na kupakiwa bodaboda kuondoka eneo la tukio bila dereva wa bodaboda kujua amebeba mjumbe wa NEC na mtuhumiwa wa rushwa!
T 671 BQL aina ya Nissan X-TRAIL NAYO ILIHUSIKAKATIKA TUKIO HILO,hapa linatimua mbio baada ya ishu nzima kubumburuka
Afisa usalama mmoja nae alidandia bodaboda na kuanza kumfukuza. Baada ya mwendesha bodaboda kujua anakimbizwa aliingia kwenye njia isiyotoka na hapo Ndio Ramesh alipotiwa nguvuni.
Mdau wetu alifika eneo la tukio na kuongea na mashuhuda kuthibitisha tukio hili. Pamoja na picha za nyumba hiyo pugu kigogo karibu na Check Point
Katika hali ya kujihami na kujisafisha Ramesh Patel amekana kuhusika katika tukio hilo ingawa ushahidi upo mfano picha hizi hapa chini baada ya kukamatwa siku ya tukkio eneo la check point pugu Dar es Salaam na Maofisa wa TAKUKURU.