LOWASSA Awa Gumzo Tena Upya!

6Mke wa Edward Lowassa, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Hakuna ubishi kuwa jina la Edward Lowassa limepamba vichwa vya habari nchini kwa miezi kadhaa huku gumzo jipya kumhusu mwanasiasa huyo likitokana na safari yake ya kuelekea muungano wa nyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangazwa.

Lowassa alitajwa juzi jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alipozungumza na waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya chama mshirika wa muungano huo cha Wananchi (Cuf) kwa lengo la kukaribishwa.

Baada ya taarifa hiyo kuenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mjadala mpya ulizuka miongoni mwa wananchi kwa kila mmoja kujaribu kuelezea hatima ya mwanasiasa huyo maarufu nchini.

“Walimwaga mboga, kamwaga ugali, mwaka huu kitaeleweka, CCM kimeuza silaha,” John Peter aliandika ujumbe huu katika akaunti yake ya Twitter.

Wakati John akiandika hivyo, Kidoti Mercy kwenye akaunti yake ya Facebook aliandika: “Chadema nimewapenda bureeee, mwaaaaa kwa kumpa nafasi Lowassa, sasa kauli mbiu chagua Lowassa kwa maendeleo ya nchi.”

Aidha, Amir Amir aliandika kwenye Facebook yake: “Chadema waliomnadi Lowassa kama fisadi papa leo anakuwa mgombea wao, aibu yao.”

Mbali na mijadala hiyo kwenye mitandao ya kijamii, gumzo juu ya mwanasiasa huyo lilitawala kwenye mitaa mbalimbali jijini Dar kwa baadhi ya watu kusema kuwa kuhamia kwake Ukawa kajimaliza kisiasa huku wengine wakisema anaweza kuingia ikulu kwa sababu ana mtaji wa watu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini