BALAA! Shamsa Ford, Davina wa BongoMovies Waangusha Sebene la Nguvu!

Shamsa_Ford_04Shamsa Ford.
Masistaduu wawili wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na Halima Yahya ‘Davina’ wameangusha sebene la nguvu katika Viwanja vya Ngome Kongwe walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF).
DAVINA11Halima Yahya ‘Davina’.
Katika tukio hilo lililojiri wikiendi iliyopita, wasanii hao walikuwa wakiburudika na Wimbo wa Nani Kama Mama wa Christian Bella uliowafanya walisakate sebene vya kutosha huku baadhi ya watu waliokuwa pembeni yao wakiangalia burudani jukwaani kuacha na kuwatazama wao.
Kucheza kwa wasanii hao kuliwahamasisha wengine kuinuka kwenye viti na kuanza kucheza huku baadhi ya watu wakiwazunguka na kuwashangilia na wengine kuwarushia fedha.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini