WANACHAMA HAWA WA CCM WAMFUATA LOWASSA CHADEMA!

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa alipokuwa anaingia ukumbini kutangaza kuhama CCM na kujiunga na Chadema
SIKU moja baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa kujiunga na Chadema, wanachama 54 wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Tawi la Mlimwa Kusini, Kata ya Ipagala mkoni hapa, Yahaya Said, wamemfuata.  

Akizungumza wakati akiwapokea wanachama hao, Katibu wa Chadema wa wilaya hiyo, Vicent Emmanuel, amesema watawapa ushirikiano wa kutosha wanachama wote wapya wanaojiunga na chama hicho.
“Mwenyekiti wa Tawi amejiunga na chama chetu na kuomba kugombea udiwani katika kata ya Mbagala,” amesema.
Amesema jumla ya watu watano wametangaza nia ya kuwania udiwani katika Kata hiyo ya Mbagala. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Jella Mambo, amesema kura za maoni za wagombea udiwani zitafanyika Julai 30 na 31 katika kata zote mkoani hapa.
“Baada ya kumaliza kura za maoni tutaenda na uamuzi kwenye vikao vya juu vya uteuzi,”amesema. 
Kwa upande wake, Said amesema ameamua kuondoka CCM kutokana na ubabaishaji na chama kuonekana kama ni mali ya mtu binafsi.
“Tukiangalia kwenye Bunge wabunge wanaotetea maslahi ya wananchi ni kutoka upinzani na wabunge wa CCM wamekuwa wakitetea maovu,” amesema
 Naye Mwenyekiti wa CUF kata ya Ipagala, wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Ismail Seif, amesema hayo ni matunda mazuri ya umoja wa vyama vinne vya upinzani.
“Wananchi wa tumeelimishwa kujua nini kinachofanyika katika umoja wetu nao wamepata nguvu ya kujiunga na chama,” amesema.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini