MAKAVU LIVE! Hongera WEMA, DIAMOND Acha Tabia za Kiswazi!

KWENU mastaa wawili wenye ‘taito’ ya juu ndani ya Bongo, Wema Isaack Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’, mambo vipi? Mko poa? diamond11

Binafsi mimi ni mzima wa afya, namshukuru Mungu, naendelea na majukumu yangu kama kawaida. Jukumu nililonalo kupitia ukurasa huu ni kuwakumbuka kupitia barua hii.
Wema-Sepetu-akina-na-mama-yake
Nikianza na Madam, kwanza nakupongeza sana kwa hatua uliyofikia kisiasa. Umepata kura 90 na umejitokeza kwa mara ya kwanza kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum. Hongera sana!
Umeonesha mwanzo mzuri. Kwamba unaweza kuwashawishi wajumbe, wakakuamini unaweza kuwatumikia, ni jambo jema. Umethubutu kujitokeza, kweli watu wakakuona na kukupigia kura.
Wapo wengi ambao tunawajua, walijitokeza kwa mara ya kwanza kama wewe, hawakuweza kufanikisha kura kama hizo ulizopata wewe. Naamini una kitu cha kipekee ambacho Mungu amekupa, usikate tamaa, songa mbele!
Diamond-MTVBase-Red-Carpet-03Naamini ukijipanga vyema, ukalelewa vizuri katika chama, inshallah uchaguzi ujao na wewe unaweza kuuthibitishia umma kwamba unaweza kuwa kiongozi. Tena uzuri ni kwamba una mtaji mkubwa wa watu nyuma yako, ambao ni mashabiki wako.
Nikirudi kwako Nasibu, mkali wao uliyechipukia kutoka Tandale jijini Dar. Sina haja ya kukupongeza sana kwa hatua ya kunyakua tuzo za MTV Africa Music (MAMA) sababu nilishafanya hivyo wiki iliyopita. Leo nimekukumbuka tena kutokana na tabia yako ya uswahili.
Naiita tabia ya uswahili kwa sababu ya mambo mengi ya wivu, chuki zisizokuwa na msingi zinazofanyika sana mitaa ya uswahilini. Majungu huko ndiko yanakopigwa na watu kupakana matope, kukomoana na vituko vya kila aina.
Kitendo cha wewe kutupia picha ya kejeli mtandaoni mara baada ya Wema kuonekana ameshindwa kuwania ubunge ni cha kiswahili sana. Si cha kiungwana hata kidogo. Hakikupaswa kufanya na mtu mwenye taito kubwa kama yako.
Eti unawashukuru wananchi wa Singida na kueleza eti mkutane Moshi kwenye shoo ya mamisi.
diamondHukuwa na maana yoyote ya kuandika maneno hayo. Unawashukuru siku ambayo Wema ameshindwa, ili iweje? Kama kuwashukuru kwa nini hukufanya hivyo kipindi kile baada ya shoo? Huo ni ushamba!
Nakumbuka pia hata uliposhinda tuzo za MTV, ulimkejeli Jokate Mwegelo kwa kuweka video yake na kusindikiza na maneno eti “mtanyooka tu.”
Jokate alilalamika. Kimsingi hukuwa pia na sababu ya kuweka video hiyo ya zamani na kumkejeli. Huo ndio uswahili wenyewe. Wewe hao wote walishakuwa wapenzi wako, mkaachana, acha maisha yaendelee.
Fanya muziki wako, wape nafasi pia wabaki kuwa mashabiki wa muziki wako hata kama penzi lilishakufa. Usiwafanye wajute kukutana na wewe. Usiwafanye wajute kufanya kazi na wewe.
Kwa leo inatosha, niwatakie kazi njema!
Ni mimi,
Erick Evarist

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini