MADAI MAZITO: MAINDA Akimbiwa na Wanaume!
Brighton Masalu
Mwigizaji wa kitambo Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kutokana na muonekano wake wa ‘usiriaz’, imekuwa ni kinga imara inayosababisha kukimbiwa na wanaume wakware.
Akizungumza na Amani, Mainda aliyewahi kuripotiwa kutoka na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alisema wakati mwingine wanaume huangalia ‘hali ya hewa’ kwa mwanamke kabla ya kumfuata na kumueleza mambo ya uhusiano.
“Unajua usiriaz wangu huu unaniepushia mambo mengi sana, wanaume wananikimbia na wananiogopa mno, hata kama siyo mkorofi lakini wanajiuliza huyu nitamuingiaje?” alisema Mainda.