MAMBO HADHARANI! RAY KIGOSI Afichua SIRI ya CHUCHU HANS!

RAY1.jpgWaigizaji mahiri wa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wake Chuchu Hans.
 Imelda Mtema, Zanzibar
Muigizaji mahiri wa kiume hapa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’amefichua siri iliyomfanya kunasa kwa staa mwenzake Chuchu Hans, na hata kupata msukumo wa kumuweka hadharani tofauti na tabia yake ya nyuma ya kutopenda kumuanika mpenzi wake.

Akizungumza na gazeti hili akiwa kwenye tamasha la kimataifa la Filamu ‘ZIFF’ lililofanyika visiwani Zanzibar, Ray alisema kilichomsukuma kumuanika Chuchu ni mambo yake adimu ambayo huwezi kupata kwa mwanamke mwingine.

Alisema anamuona kuwa na tabia zote za mke, ndiyo maana aliweza kumtambulisha kwa jamii kwa kuwa ana imani naye kwa kila kitu hivyo yuko huru watu kumfahamu.

“Bwana huyu mwanamke ana vitu vyake adimu sana, na kwa kweli nampenda na ana chembechembe zote za kuwa mke ndiyo maana nilikuwa huru kumuweka wazi bila wasiwasi wowote,” alisema Ray ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na Johari.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini