CCM KIZUNGUMKUTI! RAFU ZATAWALA KURA ZA MAONI!
Kutokana na rafu hizo zikiwemo za kutoa rushwa na kugawa kadi kwa wanafunzi na kutoa lugha za kejeli dhidi yao wamesema wameamua kugoma huku wakitaka ufumbuzi wa suala hilo ufanyike.
Kwa upande wake kaimu katibu wa CCM wa wilaya ya Nyasa Bw. Mussa Mwevi amekiri kuwepo kwa saka ta la kuingizwa kadi kinyume na utaratibu na kwamba litashughulikiwa baada ya kupita kura za maoni Agosti moja.
Naye mkuu wa wilaya Nyasa Bi. Margaret Malenga amekana tuhuma za kumnadi Bi. Stela Manyanya huku Bi. Manyanya akisema sakata hilo la kadi na malalamiko mengine atalizungumza kwenye vikao vya chama cha mapinduzi.