Pesa za Mbunge za kuwahonga wapiga kura CCM zakamatwa na TAKUKURU


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani Maswa mkoani Simiyu inamshikilia dereva mmoja aitwaye ,Seketure Kyaliga ambaye alikuwa akiendesha gari aina ya Noah lenye amba za usajili T281BCK ambalo lilikuwa na pesa za kugawia wajumbe wa chama cha mapinduzi.

Akiongea na waandishi wa habari  mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani simiyu,Adili Elinipenda amsema kuwa dereva huyo ambaye pia ni mratibu elimu kata ya nyangokolwa wilayani Bariadi, alikamatwa majira ya saa tano usiku katika kijiji cha nguliguli wilayani maswa akiwa anaendesha gari hilo ambalo baada ya kulikagua walikuta pesa kiasi cha shilingi laki nne zenye noti mpya za elfu mbilimbili.
Amesema kuwa  baada ya maafisa hao kumhoji amekiri kuwa gari hilo lilikodiwa kugawa pesa hizo kwa wajumbe na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Maswa Peter Bunyogori ambaye pi ni mgombe wa ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.
Kufuatia hali hiyo mkuu huyo wa TAKUKURU ameonya wagombea wa vyama vyote vya siasa katika mkoa huo kuachana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwahonga wajumbe ,kuwakodia nyumba za kulala wageni na kuwapa zawadi za aina yeyote kwa ajili ya ushawishi na kwamba taasisi hiyo imejipanga vilivyo kwani haitamuone huruma mgombea yeyote hata kama anatoka chama tawala.CCM.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini