UKAWA hawa wanachama anaokuja nao LOWASSA watagombea kupitia chama gani?!

Wasalaam wanajamii!
Kwanza kabisa sina ugomvi na suala LOWASSA Kuhamia UKAWA!
Swali langu hivi; Itakuawaje kama huyu mheshimiwa sana anayo team kubwa kutoka huko chama tawala na wanahitaji nao kuyasaka mabadiliko nje ya ccm kwa muda huu ambao tayari sasa mmeshapitisha wagombea wenu kwenye kura za maoni Kufuatia mgawanyo wenu wa majimbo na huku nao wanazitaka nafasi hizo kupitia UKAWA? Je, Watakubali kubaki kua wasindikizaji tu? Wengine walikua ni wabunge tayari kwa awamu iliyopita na bado ni watendaji wazuri na baadhi yao walikua Mawaziri Watakubali kukaa bench?Je, hamuoni concentration ya Urais mnaipa nafasi sana lakini huku Chini kunaweza kua na misuguano kikubwa? Je, hili suala mnakabiliana nalo vipi mapema iwezekanavyo?

-JF

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini