Lowassa CCM basi, safari ya matumaini yahamia UKAWA, CCM je?, Mabasi ya mwendo kasi kuanza rasmi? (Audio)
Magazeti ya July 29 2015 tayari yako mtaani, yote yakiwa na vichwa vyake vikubwa vya habari. Nimekusogezea zile zote kubwakubwa za leo zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa…
Lowassa yeye na CCM basi, safari ya matumaini yahamia rasmi UKAWA asema CCMsio baba yake wala mama yake, achukuwa kadi ya uwanachama CHADEMA… CCMyasema itabaki kuwa imara Lowassa ajimaliza, waitisha mkutano muhimu na waandishi wa habari leo Dar kupitia mitandao yake ya kijamii.
TAKUKURU yadaka Wagombea Ubunge CCM jimbo la Ukonga dhidi ya vitendo vya rushwa, Vituo vya BVR vya agizwa kufungua saa moja kamili asubuhi badala ya saa mbili kamili asubuhi ili kuharakisha zoezi la uandikishaji.
Wafanyabiashara wa maeneo ya Jangwani waagizwa kubomoa vibanda vyao vya biashara…Ajali mbaya ya basi yaua Mapadri 2 jana asubuhi maeneo ya Kagera, Kundi la Panya Road wadaiwa kuvamia mitaa ya Kikogo na kupora vituo vya BVR.
Mradi wa mabasi ya mwendo kasi DALT umekamilika kwa 90% na unategemea kuzinduliwa mwezi Agosti kwa sasa wako kwenye hatua za mwisho ya kutoa huduma za mpito, route ya kwanza itakuwa kwanzia Kivukoni kwenda Kimara.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti @Clouds.fm nimekurekodia na kukusogezea hapa chini.