VIDEO&PICHAZ: Huwezi Amini! Dereva Hakushtuka Mpaka Hili Basi Likaja Kunasa Hapa Chini ya Daraja Ufaransa…

Basi Ajali II

Kama kuna ajali ambazo zimewahi kunishtua ni hii hapa, kwanza najiuliza dereva hakuona au ilikuwaje mpaka hii basi ikanasa hapa!
Ndani ya Basi kulikuwa na Wanafunzi 60 wa Kihispania, wametoka zao Bilbao kwenda Amsterdam bahati mbaya hii ajali ikatokea wakiwa eneo la La Madeleine, Ufaransa… Mwanafunzi mmoja amesema wengi wao walikuwa wamelala ndani ya basi, wakashtukia tu gari imenasa chini ya daraja na imekatika sehemu yote ya juu.
Majeruhi wengi walikuwa waliokaa kwenye siti ya nyuma, walipelekwa Hospitali na wengine ilibidi waahirishe tour yao na kurudi nyumbani kwao Hispania.
Basi Ajali
Dereva alikamatwa na kupimwa wakakuta hakuwa amelewa wala hakuwa na tatizo lolote, alichojitetea ni kwamba alikuwa akifata maelekezo ya barabara kwa kutumia GPS na hakuwa amegundua kwamba daraja hilo lina urefu ambao basi lake haliwezi kupita !!
Hii video hapa chini ni ajali ya aina hiyohiyo iliyotokea Uingereza 2013, basi likakatika baada ya kupita chini ya daraja la treni.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini