MASTAA Wanaomfuata LOWASSA Waonywa!
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.
Gladness Mallya
STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amewaasa mastaa waliotangaza kumfuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amehamia UKAWA hivi karibuni akitokea CCM kwamba waachane na tabia ya kufuata mkumbo.Akipiga stori na gazeti hili alisema kwamba wale mastaa wanaomfuata Lowassa wanatakiwa kuwa makini na wasikurupuke kwa kufuata mkumbo bali watafakari kwanza kwamba yeyote wanayemshabikia anafaa na atawasaidia katika maisha na kazi zao kwani wengi wanajikuta wakifuata mkumbo tu.
“Mimi sijui niko upande gani ila yeyote atakayeonekana anafaa kutuongoza sisi wananchi ndiye nitakayemsapoti, huwa sina mambo ya timu kwa kweli, nawasihi wasanii wenzangu waachane na kukurupuka katika mambo haya ya siasa,” alisema Shamsa.