Hatimaye DIAMOND PLATINUMZ Afunguka Kuhusu Wale Watoto Wake wa SHULE!
Brighton Masalu
VUNJA ukimya! Mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusiana na sakata la watoto alioahidi kuwasomesha kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya ada.
Akistorisha na Risasi Mchanganyiko ndani ya Hoteli ya Ntansoma jijini Dar alipokuwa akiwashukuru Watanzania kwa kumwezesha kutwaa Tuzo ya MTV Africa (Mama), Diamond alisema kilichotokea ni tamaa ya mtu aliyemkabidhi jukumu la kusimamia ada na mahitaji yote ya shuleni ya watoto hao.
Diamond alifunguka kuwa kutokana na kumwamini mtu huyo na yeye kuwa ‘bize’, alishindwa kupata muda wa kufuatilia kwa ukaribu sakata hilo hadi aliposhtushwa na habari iliyoripotiwa na gazeti hili.
“Nilisiktishwa sana, nilitoa fedha zote, nikampa mtu ambaye nilimuamini sana lakini kwa tamaa zake akaamua kuzitumia fedha hizo, unajua muda wangu ni mchache sana, hivyo sikufuatilia, lakini kwa sasa mambo yote yamekaa sawa,” alisema Diamond.