Kisa LOWASSA...Jacqueline Wolper Achukua Umuzi Huu!
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’.
Imelda Mtema
KAZI ipo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’ kuamua kushonesha vazi maarufu (gwanda) la Chama cha Demokrasia na Maendeleo, chama ambacho mfuasi wake, Edward Lowassa amejiunga nacho Jumanne iliyopita.

Mara baada ya Lowassa ambaye aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM kuhamia Chadema kinachounda umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Wolper alitangaza kusaka fundi wa gwanda katika mitandao ya kijamii, akafanikiwa.
“Nina furaha ya aina yake, baba (Lowassa) katoka CCM nami naungana naye katika maisha mapya ya Chadema hivyo nimeshapata fundi, ananishonea gwanda soon nalitinga,” alisema Wolper.