HUWEZI AMINI! KUKATWA KWA WEMA SEPETU NI KICHEKO KWA STAA MWENZAKE HUYU BONGO MUVI!

BABA HAJI NA WEMA (1)Staa wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ akipozi.
 STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.
BABA HAJI NA WEMA (2)Wema Sepetu.
Akionekana mwenye furaha huku akiserebuka muziki alisema kuwa mbunge wenu amekosa ubunge, jambo lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa inafahamika kuwa ana bifu naye.
“Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenu kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.
Bifu la Baba Haji na Wema lilianza kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini