KUMEKUCHA! LOWASSA AFUNGUKA MAZITO WAKATI AKITANGAZA KUHAMIA CHADEMA RASMI LEO
Lowassa ametoa kauli hii Bahari Beach , Dar akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa UKAWA ambao wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia hatima yake kuelekea ikulu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Lowassa amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha, ameamua kujiondoa CCM kwa kuwa siyo baba yake wala mama yake na kuitikia wito wa UKAWA kupitia CHADEMA.
Amesema safari yake haitafanikiwa iwapo hatajitokeza watu wengi kupiga kura na anaiomba tume ya uchaguzi iongeze muda ili watu wote waweze kujiandikisha
Lowassa amesema alinyimwa haki yake na CCM kama mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakuwa mnafiki akisema ana imani na chama hicho
Baada ya maelezo hayo; Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe alisimama na kumkabidhi rasmi Lowassa Kadi ya CHADEMA.