Juma Nature ameahidi kujenga msikiti pamoja na madrasa ya watoto kujifunza imani na misingi ya kiislamu.

Juma Nature na waumini wa dini ya kiislam

Akizungumza na Bongo5 juzi nyumbani kwake baada ya kufuturisha, Nature alisema anafikiria vitu vingi vya kuifanyia jamii ila tatizo ni pesa ndizo zinakwamisha malengo hayo.

Juma Nature


“Kitu kikubwa kinachosumbumbua ni pesa, kwa sababu pesa ndio kila kitu ili uweze kuwafanyia waislamu wenzako vitu vizuri kama kujenga misikiti, kujenga madrasa, kuwatafuta waalimu, kwa sababu walimu lazima walipwe kwanza,” alisema Nature.

“Mimi nitakapokuwa vizuri na kwa jinsi Mungu anavyotaka, nitajenga, nikishakuwa na pesa yangu nimeshatoa nadhiri kwa mwenyezi Mungu, Mungu ukinijalia pesa fulani ambayo nimeishaweka kichwani, nitafanya kitu kikubwa sana, na kwakuwa hiki kidogo alichonipa nimeweza kufanya kitu kama hiki (kufturisha) japo kuwa sina hela lakini nimeweza kufanya, sasa imagine kama nitakuwa na mahela yangu kama wenzetu hawa unawasikia, mara wako South Africa kula bata, wanatumia pesa kwa sifa. Mimi nitaenda out ya hiyo kitu, sitaki kuzungumzia sana suala hili lakini namwachia Mungu anizidishie maisha marefu yenye baraka tele kabisa na tuendelee kuishi kwa amani na upendo na tumtumikie Mungu.”

Hizi ni picha za shughuli hiyo.

Juma Nature akiwa na mashehe pamoja na waumini wa dini ya kiislam

Nature na waumini wa dini ya kiislam

Juma Nature akiwa na watoto wa madrasa

Juma Nature akiwa nyumbani kwake

Nature akifanya dua baada ya kufturisha

Wadau mbalimbali wakifturu







Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini